1
Luka 21:36
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Hivyo, iweni tayari kila wakati. Ombeni ili muepuke mambo haya yote yatakayotokea na mweze kusimama kwa ujasiri mbele za Mwana wa Adamu.”
Compara
Explorar Luka 21:36
2
Luka 21:34
Iweni waangalifu, msiutumie muda wenu katika sherehe za ulevi na kuhangaikia maisha haya. Mkifanya hivyo, hamtaweza kufikiri vyema na mwisho unaweza kuja mkiwa hamjajiandaa.
Explorar Luka 21:34
3
Luka 21:19
Mtayaokoa maisha yenu ikiwa mtaendelea kuwa imara katika imani mnapopita katika mambo haya yote.
Explorar Luka 21:19
4
Luka 21:15
Nitawapa hekima kusema mambo ambayo adui zenu watashindwa kuyajibu.
Explorar Luka 21:15
5
Luka 21:33
Ulimwengu wote, dunia yote na anga vitapita, lakini maneno yangu yataishi milele.
Explorar Luka 21:33
6
Luka 21:25-27
Mambo ya kushangaza yatatokea kwenye jua, mwezi na nyota na watu katika dunia yote wataogopa na kuchanganyikiwa kutokana na kelele za bahari na mawimbi yake. Watazimia kwa hofu na kuogopa watakapoona mambo yanayoupata ulimwengu. Kila kitu katika anga kitabadilishwa. Kisha watu watamwona Mwana wa Adamu akija katika wingu mwenye nguvu na utukufu mwingi.
Explorar Luka 21:25-27
7
Luka 21:17
Kila mtu atawachukia kwa sababu mnanifuata mimi.
Explorar Luka 21:17
8
Luka 21:11
Kutakuwa matetemeko makubwa, kutakuwa njaa na magonjwa ya kutisha sehemu nyingi. Mambo ya kutisha yatatokea, na mambo ya kushangaza yatatokea kutoka mbinguni ili kuwaonya watu.
Explorar Luka 21:11
9
Luka 21:9-10
Mtakaposikia kuhusu vita na machafuko, msiogope. Mambo haya lazima yatokee kwanza. Lakini mwisho hautakuja haraka.” Kisha Yesu akawaambia, “Mataifa yatapigana na mataifa mengine. Falme zitapigana na falme zingine.
Explorar Luka 21:9-10
10
Luka 21:25-26
Mambo ya kushangaza yatatokea kwenye jua, mwezi na nyota na watu katika dunia yote wataogopa na kuchanganyikiwa kutokana na kelele za bahari na mawimbi yake. Watazimia kwa hofu na kuogopa watakapoona mambo yanayoupata ulimwengu. Kila kitu katika anga kitabadilishwa.
Explorar Luka 21:25-26
11
Luka 21:10
Kisha Yesu akawaambia, “Mataifa yatapigana na mataifa mengine. Falme zitapigana na falme zingine.
Explorar Luka 21:10
12
Luka 21:8
Yesu akasema, “Iweni waangalifu, msije mkarubuniwa. Watu wengi watakuja wakitumia jina langu, watasema, ‘Mimi ndiye Masihi,’ na ‘Wakati sahihi umefika!’ Lakini msiwafuate.
Explorar Luka 21:8
Inici
La Bíblia
Plans
Vídeos