1
Marko 5:34
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Kisha Yesu akamwambia, “Binti yangu imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, na uendelee kupona matatizo yako.”
Compara
Explorar Marko 5:34
2
Marko 5:25-26
Alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa akitoka damu (kama ilivyo desturi ya wanawake kila mwezi) kila siku kwa miaka kumi na miwili. Huyu alikuwa ameteseka sana akiwa chini ya uangalizi wa madaktari wengi. Yeye alikuwa ametumia vyote alivyokuwa navyo. Hata hivyo hali yake iliendelea kuwa mbaya zaidi.
Explorar Marko 5:25-26
3
Marko 5:29
Mara moja chanzo cha kutoka kwake damu kikakauka, na akajisikia mwilini mwake kwamba amepona matatizo yake.
Explorar Marko 5:29
4
Marko 5:41
akaushika mkono wa mtoto yule na kumwambia “ Talitha koum! ” (maana yake, “Msichana mdogo, ninakuambia amka usimame!”)
Explorar Marko 5:41
5
Marko 5:35-36
Wakati alipokuwa akizungumza haya watumishi walikuja kutoka nyumbani kwa afisa wa sinagogi. Nao wakamwambia yule afisa, “Binti yako amefariki kwa nini uendelee kumsumbua huyo mwalimu?” Lakini Yesu aliyasikia yale waliyokuwa wakisema, na akamwaambia yule afisa wa sinagogi, “Usiogope. Amini tu.”
Explorar Marko 5:35-36
6
Marko 5:8-9
Yule pepo alisema haya kwa sababu Yesu alikuwa anamwambia, “Mtoke huyo mtu, ewe pepo mchafu!” Ndipo Yesu akamwuliza yule mtu, “Jina lako nani?” Naye akamjibu, “Jina langu ni Jeshi, kwa sababu tuko wengi.”
Explorar Marko 5:8-9
Inici
La Bíblia
Plans
Vídeos