Mattayo MT. 10

10
1AKAWAITA wanafunzi wake thenashara, akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, wawafukuze, na kuponya magonjwa yote na dhaifu zote.
2Na majina ya mitume thenashara ni haya: Wa kwanza Simon aliyekwitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake; 3Filipo, na Bartolomayo, na Tomaso, na Mattayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Lebbayo, aliyekwitwa Thaddayo; 4Simon Kananayo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.
5Hawa thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akinena, Katika njia ya Mataifa msiende, wala mjini mwa Wasamaria msiingie: 6afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 7Na katika kuenenda kwenu, khubirini, nikinena, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8Ponyeni wagonjwa, takaseni wenye ukoma, fufueni wafu, fukuzeni pepo; mmepata burre, toeni burre. 9Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba mishipini mwenu; 10wala mkoba wa safari, wula kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo: maana mtenda kazi astahili posho lake. 11Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu amini; kakaeni humo hatta mtakapotoka. 12Na mkiingia katika nyumba, isalimuni. 13Na nyumba ile ikistahili, amani yenu iifikilie: la, haistahili, amani yenu iwarudieni. 14Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu. 15Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule.
16Angalieni, mimi nawatumeni kama kondoo kati ya mbwa wa mwitu: bassi mwe na busara kama nyoka, na msio na dhara kama hua. 17Jihadharini na wana Adamu; kwa maana watawapelekeni mbele ya baraza, na katika masunagogi yao watawapiga; 18nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. 19Lakini hapo wakatapowapelekeni, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. 20Kwa kuwa si ninyi msemao, bali Roho ya Baba yenu asemae ndani yenu. 21Na ndugu atamsaliti ndugu apate kufa, na baba atamsaliti mtolo; na watoto wataondoka kuwashitaki wazee wao, wawafishe. 22Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka. 23Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine: kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza miji yote ya Israeli, hatta ajapo Mwana wa Adamu.
24Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumishi hampiti bwana wake. 25Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebul, je, si zaidi wale walio nyumbani mwake? 26Bassi, msiwaogope, kwa maana hakuna jambo lililostirika, ambalo halitafunuliwa baadae; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana baadae. 27Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni kalika nuru; na msikialo kwa siri, likhubirini juu ya nyumba. 28Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum.
29Videge viwili haviuzwi kwa pesa moja? Na hatta mmoja haanguki chini asijiojua Baba yemi: 30hatta na nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. 31Msiogope bassi; hora ninyi kuliko videge vingi. 32Bassi killa mtu atakaenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33Bali mtu ye yote atakaenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
34Msidhani ya kuwa nalikuja kueneza amani duniani; la! sikuja kueneza amani, bali upanga. 35Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na baba yake, na binti na mama yake, na mkwe na mkwe mtu: 36na adui wa mtu ndio wale wa nyumbani mwake. 37Apendae baba au mama kuliko mimi, hanifai; na apendae mwana au binti kuliko mimi hanifai. 38Nae asiyechukua msalaba wake na kufuata nyuma yangu, hanifai. 39Anaeipata roho yake ataiangamiza; nae anaeitoa roho yake kwa ajili yangu ataipata.
40Awapokeae ninyi, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenituma. 41Ampokeae nabii kwa kuwa yu nabii, atapata thawabu ya nabii; nae ampokeae mwenye haki kwa kuwa yu mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. 42Na mtu aliye yote atakaemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji ya baridi tu, kwa kuwa yu mwanafunzi, amin, nawaambieni, haitampotea kamwe thawabu yake.

S'ha seleccionat:

Mattayo MT. 10: SWZZB1921

Subratllat

Comparteix

Copia

None

Vols que els teus subratllats es desin a tots els teus dispositius? Registra't o inicia sessió