1 Mose 11
11
Jengo la mnara wa Babeli.
(Taz. 1 Mambo 1:24-27.)
1Watu wa nchi yote nzima walikuwa wenye msemo mmoja, nayo maneno yalikuwa yaleyale mamoja. 2Ikawa, walipoondoka kwenda upande wa maawioni kwa jua, wakaona bonde pana katika nchi ya Sinari, wakakaa huko. 3Kisha wakasemezana wao kwa wao: Haya! Na tuumbe matofali, tuyachome moto! Haya matofali yakawa mawe yao ya kujenga, nao udongo ukawa chokaa yao. 4Wakasema: Haya! Na tujijengee mji wenye mnara, nayo ncha yake ifike mbinguni, tujipatie jina, tusije kusambazwa katika nchi zote za duniani!
Mungu anaivuruga misemo ya watu.
5Ndipo, Bwana aliposhuka, autazame huo mji na mnara, wana wa Adamu walioujenga.#1 Mose 18:21; Sh. 14:2; 18:10. 6Bwana akasema: Ninawaona watu hawa kuwa ukoo mmoja tu, nao msemo wao wote ni mmoja tu vilevile. Nao huu ndio mwanzo tu wa matendo yao; sasa yote, watakayoyawaza mioyoni kuyafanya, hakuna lo lote litakalowashinda. 7Haya! Na tushuke, tuuvuruge msemo wao huko, mtu asiusikie msemo wa mwenziwe! 8Hivyo ndivyo, Bwana alivyowatawanya na kuwatoa huko, wajiendee kukaa katika nchi zote. Ndipo, walipoacha kuujenga ule mji.#Luk. 1:51. 9Kwa sababu hiyo wakauita jina lake Babeli (Mvurugo), kwa kuwa huko ndiko, Bwana alikouvuruga msemo wa watu wote wa huku nchini, akawatawanya na kuwatoa huko, wajiendee kukaa katika nchi zote.
Vizazi vya Semu mpaka Aburahamu.
10Hivi ndivyo vizazi vya Semu: Semu alipokuwa mwenye miaka 100 akamzaa Arpakisadi katika mwaka wa pili baada ya mafuriko ya maji.#1 Mose 10:22; Luk. 3:36. 11Semu alipokwisha kumzaa Arpakisadi akawapo miaka 500, akazaa wana wa kiume na wa kike. 12Arpakisadi alipokuwa mwenye miaka 35 akamzaa Sela. 13Arpakisadi alipokwisha kumzaa Sela akawapo miaka 403, akazaa wana wa kiume na wa kike. 14Sela alipokuwa mwenye miaka 30 akamzaa Eberi. 15Sela alipokwisha kumzaa Eberi akawapo miaka 403, akazaa wana wa kiume na wa kike. 16Eberi alipokuwa mwenye miaka 34 akamzaa Pelegi. 17Eberi alipokwisha kumzaa Pelegi akawapo miaka 430, akazaa wana wa kiume na wa kike. 18Pelegi alipokuwa menye miaka 30 akamzaa Reu. 19Pelegi alipokwisha kumza Reu akawapo miaka 209, akazaa wana wa kiume na wa kike. 20Reu alipokuwa mwenye miaka 32 akamzaa Serugi. 21Reu alipokwisha kumzaa Serugi akawapo miaka 207, akazaa wana wa kiume na wa kike. 22Serugi alipokuwa mwenye miaka 30 akamzaa Nahori. 23Serugi alipokwisha kumzaa Nahori akawapo miaka 200, akazaa wana wa kiume na wa kike. 24Nahori alipokuwa mwenye miaka 29 akamzaa Tera. 25Nahori alipokwisha kumzaa Tera, akawapo miaka 119, akazaa wana wa kiume na wa kike. 26Tera alipokuwa mwenye miaka 70 akamzaa Aburamu na Nahori na Harani.
27Hivi ndivyo vizazi vya Tera: Tera akamzaa Aburamu na Nahori na Harani. Naye Harani akamzaa Loti. 28Harani akafa machoni pake baba yake Tera katika nchi alikozaliwa, ndiko Uri wa Wakasidi. 29Kisha Aburamu na Nahori wakajichukulia wanawake, mkewe Aburamu jina lake Sarai, naye mkewe Nahori jina lake Milka, binti Harani aliyekuwa baba yao Milka na Isika.#1 Mose 22:20. 30Lakini Sarai alikuwa mgumba, asipate mtoto. 31Kisha Tera akamchukua mwanawe Aburamu na Loti, mwana wa mwanawe Harani, na mkwewe Sarai, mkewe mwanawe Aburamu, wakatoka naye mle Uri wa Wakasidi kwenda katika nchi ya Kanaani, nao walipofika Harani wakakaa huko.#Yos. 24:2; Neh. 9:7. 32Nazo siku zake Tera zilikuwa miaka 205, naye akafa huko Harani.
S'ha seleccionat:
1 Mose 11: SRB37
Subratllat
Comparteix
Copia
Vols que els teus subratllats es desin a tots els teus dispositius? Registra't o inicia sessió
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: