YouVersion Logo
Search Icon

Mwanzo 10

10
Mataifa Yaliyotokana Na Nuhu
(1 Nyakati 1:5-23)
1 Hawa ndio wazao wa Nuhu: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.
Wazao Wa Yafethi
2 Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
3 Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
4 Wana wa Yavani walikuwa:
Al-Yasa, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. 5(Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)
Wazao Wa Hamu
6 Wana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misraimu,#10:6 Yaani Misri. Putu na Kanaani.
7 Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. 9 Alikuwa mwindaji hodari mbele za bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za bwana.” 10 Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. 11 Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, 12na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.
13Misraimu alikuwa baba wa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 14 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
15 Kanaani alikuwa baba wa:
Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, 16 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 17 Wahivi, Waariki, Wasini, 18 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, 19 na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.
20Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
Wazao Wa Shemu
21 Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.
22 Wana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
23 Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
24 Arfaksadi alikuwa baba wa Shela,
naye Shela akamzaa Eberi.
25Eberi akapata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
26Yoktani alikuwa baba wa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 27 Hadoramu, Uzali, Dikla, 28 Obali, Abimaeli, Sheba, 29 Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
30Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.
31Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
32Hizi ndizo koo za wana wa Nuhu, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.

Currently Selected:

Mwanzo 10: NMM

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in