Luka 23
23
Pilato amhoji Isa
(Mathayo 27:1-2, 11-14; Marko 15:1-15; Yohana 18:28–19:16)
1Kisha umati wote wa watu wakainuka na kumpeleka Isa kwa Pilato. 2Nao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita ni Al-Masihi#23:2 Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta., mfalme.”
3Basi Pilato akamuuliza Isa, “Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?”
Isa akajibu, “Wewe wasema.”
4Pilato akawaambia viongozi wa makuhani na umati ule wote, “Sioni msingi wowote wa kumshtaki mtu huyu!”
5Lakini wao wakakazana kusema, “Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika Yudea yote, tangu Galilaya alikoanzia, hadi sehemu hii!”
Isa apelekwa kwa Herode
6Pilato aliposikia hayo akauliza kama huyo mtu alikuwa Mgalilaya. 7Alipofahamu kwamba Isa alikuwa chini ya mamlaka ya Herode, akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa pia Yerusalemu.
8Herode alipomwona Isa alifurahi sana, kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amesikia mambo mengi kumhusu. Pia alitarajia kumwona akifanya miujiza kadha wa kadha. 9Herode akamuuliza maswali mengi, lakini Isa hakumjibu lolote. 10Wakati huo viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walikuwa wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. 11Herode na askari wake wakamdhihaki Isa na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato. 12Siku hiyo, Herode na Pilato wakapata urafiki; kabla ya jambo hili walikuwa na uadui kati yao.
Isa ahukumiwa kifo
(Mathayo 27:15-26; Marko 15:6-15; Yohana 18:39–19:16)
13Basi Pilato akawaita pamoja viongozi wa makuhani, viongozi wengine na watu, 14akawaambia, “Ninyi mlimleta huyu mtu kwangu kana kwamba ni mtu anayewachochea watu ili waasi. Nimemhoji mbele yenu nami sikupata msingi wowote wa mashtaka yenu dhidi yake. 15Wala Herode hakumpata na kosa lolote, ndiyo sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lolote linalostahili kifo. 16Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi na kumwachilia.” [ 17Kwa kuwa ilikuwa lazima kuwafungulia mfungwa mmoja wakati wa Sikukuu.]#23:17 Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.
18Ndipo watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “Mwondoe mtu huyu! Tufungulie Baraba!” 19(Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa sababu ya maasi yaliyokuwa yametokea mjini, na kwa ajili ya uuaji.)
20Pilato, akitaka kumwachia Isa, akasema nao tena. 21Lakini wao wakaendelea kupiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!”
22Kwa mara ya tatu, Pilato akawauliza, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yoyote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi, na kisha nitamwachia.”
23Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu, wakidai kwamba Isa asulubiwe. Hivyo, kelele zao zikashinda. 24Kwa hiyo Pilato akatoa hukumu kwamba madai yao yatimizwe. 25Akamfungua yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika uasi dhidi ya serikali na mauaji. Akamkabidhi Isa mikononi mwao, wamfanyie watakavyo.
Isa asulubishwa
(Mathayo 27:32-44; Marko 15:21-32; Yohana 19:17-27)
26Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni Mkirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Isa. 27Idadi kubwa ya watu wakamfuata Isa, wakiwamo wanawake waliokuwa wakimlilia na kumwombolezea. 28Isa akawageukia, akawaambia, “Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi bali jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29Kwa maana wakati utafika mtakaposema, ‘Wamebarikiwa wanawake tasa, ambao tumbo zao hazikuzaa, wala matiti yao hayakunyonyesha!’ 30Ndipo
“ ‘wataiambia milima, “Tuangukieni!”
na vilima, “Tufunikeni!” ’
31Kwa maana kama wamefanya hivi kwa mti mbichi, kwa mti mkavu itakuwaje?”
32Watu wawili wahalifu walipelekwa pamoja na Isa ili wakasulubiwe. 33Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walimsulubisha Isa pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume, na mwingine upande wake wa kushoto. 34Isa akasema, “Baba#23:34 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu., wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.
35Watu wakasimama hapo wakimwangalia, nao viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama yeye ndiye Al-Masihi wa Mungu, Mteule wake.”
36Askari nao wakaja, wakamdhihaki. Wakamletea siki ili anywe, 37na wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.”
38Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya:
Huyu ndiye
Mfalme wa Wayahudi.
39Mmoja wa wale wahalifu waliosulubiwa pamoja naye akamtukana, akasema: “Wewe si ndiye Al-Masihi? Jiokoe mwenyewe na utuokoe na sisi.”
40Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akasema, “Je, wewe humwogopi Mungu, wakati uko kwenye adhabu hiyo hiyo? 41Sisi tumehukumiwa kwa haki kwa kuwa tunapata tunayostahili kwa ajili ya matendo yetu. Lakini huyu mtu hajafanya kosa lolote.”
42Kisha akasema, “Isa, unikumbuke utakapokuja katika ufalme wako.”
43Isa akamjibu, “Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami Paradiso.#23:43 Paradiso maana yake bustani nzuri; hapa ni mahali zinapoenda roho za watakatifu.”
Kifo cha Isa
(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Yohana 19:28-30)
44Ilikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa, 45kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili. 46Isa akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.
47Yule jemadari alipoona yaliyotukia, akamsifu Mungu, akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48Watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao. 49Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wale wanawake waliokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyatazama mambo haya.
Maziko ya Isa
(Mathayo 27:57-61; Marko 15:42-47; Yohana 19:38-42)
50Basi kulikuwa na mtu mmoja mwema na mwenye haki, jina lake Yusufu. Yeye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wayahudi#23:50 Baraza la Wayahudi ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu., 51lakini yeye hakuwa amekubaliana na maamuzi na vitendo vya viongozi wenzake. Huyu alikuwa raia wa Arimathaya huko Yudea, naye alikuwa anaungojea ufalme wa Mungu kwa matarajio makubwa. 52Yusufu alienda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Isa. 53Akaushusha kutoka msalabani, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, na kuuweka katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limezikiwa mtu mwingine bado. 54Ilikuwa Siku ya Maandalizi, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza.
55Wale wanawake waliokuwa wamekuja pamoja na Isa wakimfuata kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Isa ulivyolazwa. 56Kisha wakarudi nyumbani, wakaandaa manukato na marhamu ya kuupaka huo mwili. Lakini wakapumzika siku ya Sabato kama ilivyoamriwa.
Currently Selected:
Luka 23: ONMM
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.

: