1
Yohana 11:25-26
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Isa akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi; na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?”
Vertaa
Tutki Yohana 11:25-26
2
Yohana 11:40
Isa akamwambia, “Sikukuambia kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”
Tutki Yohana 11:40
3
Yohana 11:35
Isa akalia machozi.
Tutki Yohana 11:35
4
Yohana 11:4
Lakini Isa aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti, bali ni wa kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.”
Tutki Yohana 11:4
5
Yohana 11:43-44
Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti yake, akaita, “Lazaro, njoo huku!” Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Isa akawaambia, “Mfungueni; mwacheni aende zake.”
Tutki Yohana 11:43-44
6
Yohana 11:38
Isa akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana kwa mara nyingine. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe liliwekwa kwenye ingilio lake.
Tutki Yohana 11:38
7
Yohana 11:11
Baada ya kusema haya, Isa akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha.”
Tutki Yohana 11:11
Koti
Raamattu
Suunnitelmat
Videot