1
Yohana 13:34-35
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu 2024
“Amri mpya nawapa: Mpendane. Kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. Mkipendana ninyi kwa ninyi kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”
השווה
חקרו Yohana 13:34-35
2
Yohana 13:14-15
Kwa hiyo, ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi. Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi.
חקרו Yohana 13:14-15
3
Yohana 13:7
Isa akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.”
חקרו Yohana 13:7
4
Yohana 13:16
Amin, amin nawaambia, mtumishi si mkuu kuliko bwana wake, wala aliyetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma.
חקרו Yohana 13:16
5
Yohana 13:17
Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri kwenu mkiyatenda.
חקרו Yohana 13:17
6
Yohana 13:4-5
aliondoka chakulani, akavua vazi lake la nje, akajifunga kitambaa kiunoni. Kisha akamimina maji kwenye sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni.
חקרו Yohana 13:4-5
בית
כתבי הקודש
תכניות
קטעי וידאו