Mwanzo 2
2
1Basi mbingu na nchi zikamalizika kuumbwa, na jeshi lake lote. 2#Kut 31:17; Ebr 4:4,10 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3#Kut 16:22-30 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. 4Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilivyoumbwa.
Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi 5#Zab 104:14; 65:9,11 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; 6maji yakapanda katika nchi, yakatia unyevu juu ya uso wote wa ardhi. 7#1 Kor 15:45 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai. 8#Mwa 13:10 BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya. 9#Eze 31:8; Mwa 3:22; Ufu 2:7; 22:2,14 BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. 10#Zab 46:4 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne. 11#Mwa 25:18 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu; 12na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham. 13Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi. 14#Dan 10:4 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati. 15BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. 16BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, “Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”
18BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. 19#Zab 8:6 BWANA Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake. 20Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye. 21#Mwa 15:12 BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, 22#Mit 18:22; Ebr 13:4 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. 23#Mwa 29:14; Amu 9:2; 2 Sam 5:1; Efe 5:30; 1 Kor 11:8 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. 24#Zab 45:10; Mt 19:5; Mk 10:7-8; 1 Kor 6:16; Efe 5:28-31 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. 25#Kut 32:25; Isa 47:3 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
נבחרו כעת:
Mwanzo 2: SRUVDC
הדגשה
שתף
העתק
רוצים לשמור את ההדגשות שלכם בכל המכשירים שלכם? הירשמו או היכנסו
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.