1
Luka 6:38
Neno: Maandiko Matakatifu
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.”
तुलना
खोजें Luka 6:38
2
Luka 6:45
Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka kwenye hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo maovu kutoka kwenye hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake.
खोजें Luka 6:45
3
Luka 6:35
Lakini wapendeni adui zenu, watendeeni mema, wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo thawabu yenu itakapokuwa kubwa, nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu Sana, kwa sababu yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na kwa wale waovu.
खोजें Luka 6:35
4
Luka 6:36
Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
खोजें Luka 6:36
5
Luka 6:37
“Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa. Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa. Sameheni, nanyi mtasamehewa.
खोजें Luka 6:37
6
Luka 6:27-28
“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.
खोजें Luka 6:27-28
7
Luka 6:31
Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.
खोजें Luka 6:31
8
Luka 6:29-30
Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyang’anya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia. Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie.
खोजें Luka 6:29-30
9
Luka 6:43
“Hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri.
खोजें Luka 6:43
10
Luka 6:44
Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba, wala zabibu kwenye michongoma.
खोजें Luka 6:44
होम
बाइबिल
योजनाएँ
वीडियो