Luka 21:25-27

Luka 21:25-27 TKU

Mambo ya kushangaza yatatokea kwenye jua, mwezi na nyota na watu katika dunia yote wataogopa na kuchanganyikiwa kutokana na kelele za bahari na mawimbi yake. Watazimia kwa hofu na kuogopa watakapoona mambo yanayoupata ulimwengu. Kila kitu katika anga kitabadilishwa. Kisha watu watamwona Mwana wa Adamu akija katika wingu mwenye nguvu na utukufu mwingi.