1
Yohana 10:10
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mwizi anakuja kuiba, kuua, na kuangamiza. Lakini mimi nilikuja kuwaletea uzima, na muwe nao kwa ukamilifu.
Confronta
Esplora Yohana 10:10
2
Yohana 10:11
Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huyatoa maisha yake kwa ajili ya kondoo.
Esplora Yohana 10:11
3
Yohana 10:27
Kondoo wangu huisikia sauti yangu. Nami nawajua, nao hunifuata.
Esplora Yohana 10:27
4
Yohana 10:28
Mimi nawapa kondoo wangu uzima wa milele. Nao hawatakufa kamwe, na tena hakuna atakayemchukua yeyote kutoka mkononi mwangu.
Esplora Yohana 10:28
5
Yohana 10:9
Mimi ni mlango. Yeyote anayeingia kupitia kwangu ataokoka. Ataweza kuingia na kutoka nje. Atapata kila anachohitaji.
Esplora Yohana 10:9
6
Yohana 10:14-15
Mimi ni mchungaji ninayewajali kondoo. Nawafahamu kondoo wangu kama ambavyo Baba ananijua mimi. Na kondoo wananijua kama nami ninavyomjua Baba. Nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo hawa.
Esplora Yohana 10:14-15
7
Yohana 10:29-30
Baba yangu ndiye aliyenipa hao, naye ni mkuu kuliko wote. Hakuna anayeweza kuwaiba kondoo wangu kutoka mkononi mwangu. Mimi na Baba tu umoja.”
Esplora Yohana 10:29-30
8
9
Yohana 10:18
Hakuna anayeweza kuuchukua uhai wangu kutoka kwangu. Nautoa uhai wangu kwa hiari yangu. Ninayo haki ya kuutoa, na ninayo haki ya kuuchukua tena. Haya ndiyo aliyoniambia Baba yangu.”
Esplora Yohana 10:18
10
Yohana 10:7
Hivyo Yesu akasema tena, “Hakika ninawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo.
Esplora Yohana 10:7
11
Yohana 10:12
Mtumishi anayelipwa ili kuwachunga kondoo yuko tofauti na mchungaji. Mtumishi wa mshahara, kondoo siyo mali yake. Hivyo anapomwona mbwa mwitu anakuja, hukimbia na kuwaacha kondoo peke yao. Mbwa mwitu huwashambulia na kuwatawanya kondoo.
Esplora Yohana 10:12
12
Yohana 10:1
Yesu akawaambia, “Hakika ninawaambia, mtu anapoingia katika zizi la kondoo, hutumia mlango. Kama akiingia kwa kutumia njia nyingine yoyote, huyo ni mwizi. Anajaribu kuwaiba kondoo.
Esplora Yohana 10:1
Home
Bibbia
Piani
Video