1
Luka 19:10
Biblia Habari Njema
Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”
比較
Luka 19:10で検索
2
Luka 19:38
wakawa wanasema: “Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana. Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!”
Luka 19:38で検索
3
Luka 19:9
Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.
Luka 19:9で検索
4
Luka 19:5-6
Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.” Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha.
Luka 19:5-6で検索
5
Luka 19:8
Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.”
Luka 19:8で検索
6
Luka 19:39-40
Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu wakamwambia Yesu, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!” Yesu akawajibu, “Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti.”
Luka 19:39-40で検索
ホーム
聖書
読書プラン
ビデオ