1
Yohana 6:35
Swahili Revised Union Version
Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.
비교
Yohana 6:35 살펴보기
2
Yohana 6:63
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Yohana 6:63 살펴보기
3
Yohana 6:27
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Yohana 6:27 살펴보기
4
Yohana 6:40
Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Yohana 6:40 살펴보기
5
Yohana 6:29
Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.
Yohana 6:29 살펴보기
6
Yohana 6:37
Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Yohana 6:37 살펴보기
7
Yohana 6:68
Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Yohana 6:68 살펴보기
8
Yohana 6:51
Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.
Yohana 6:51 살펴보기
9
Yohana 6:44
Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenituma; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Yohana 6:44 살펴보기
10
Yohana 6:33
Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.
Yohana 6:33 살펴보기
11
Yohana 6:48
Mimi ndimi chakula cha uzima.
Yohana 6:48 살펴보기
12
Yohana 6:11-12
Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee chochote.
Yohana 6:11-12 살펴보기
13
Yohana 6:19-20
Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kuikaribia mashua; wakaogopa. Naye akawaambia, Ni mimi, msiogope.
Yohana 6:19-20 살펴보기
YouVersion은 여러분의 경험을 개인화하기 위해 쿠키를 사용합니다. 저희 웹사이트를 사용함으로써 여러분은 저희의 개인 정보 보호 정책에 설명된 쿠키 사용에 동의하게 됩니다
홈
성경
묵상
동영상