1
Mwanzo 3:6
BIBLIA KISWAHILI
Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Porównaj
Przeglądaj Mwanzo 3:6
2
Mwanzo 3:1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Przeglądaj Mwanzo 3:1
3
Mwanzo 3:15
nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Przeglądaj Mwanzo 3:15
4
Mwanzo 3:16
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Przeglądaj Mwanzo 3:16
5
Mwanzo 3:19
kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Przeglądaj Mwanzo 3:19
6
Mwanzo 3:17
Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako
Przeglądaj Mwanzo 3:17
7
Mwanzo 3:11
Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
Przeglądaj Mwanzo 3:11
8
Mwanzo 3:24
Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Przeglądaj Mwanzo 3:24
9
Mwanzo 3:20
Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.
Przeglądaj Mwanzo 3:20
Strona główna
Biblia
Plany
Nagrania wideo