1
Mwanzo 3:6
Neno: Maandiko Matakatifu
Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala.
Porównaj
Przeglądaj Mwanzo 3:6
2
Mwanzo 3:1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao BWANA Mwenyezi Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”
Przeglądaj Mwanzo 3:1
3
Mwanzo 3:15
Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, yeye atakuponda kichwa, nawe utamuuma kisigino.”
Przeglądaj Mwanzo 3:15
4
Mwanzo 3:16
Kwa mwanamke akasema, “Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto. Tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala.”
Przeglądaj Mwanzo 3:16
5
Mwanzo 3:19
Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.”
Przeglądaj Mwanzo 3:19
6
Mwanzo 3:17
Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’ “Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako, kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo siku zote za maisha yako.
Przeglądaj Mwanzo 3:17
7
Mwanzo 3:11
Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”
Przeglądaj Mwanzo 3:11
8
Mwanzo 3:24
Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.
Przeglądaj Mwanzo 3:24
9
Mwanzo 3:20
Adamu akamwita mkewe Hawa, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.
Przeglądaj Mwanzo 3:20
Strona główna
Biblia
Plany
Nagrania wideo