YouVersion logo
Dugme za pretraživanje

Luka 17

17
Kuwaondolea ndugu.
1Kisha akawaambia wanafunzi wake: Makwazo hayana budi kuja, lakini anayeyaleta atapatwa na mambo. 2Akitundikwa shingoni pake jiwe kubwa la kusagia, kisha atumbukizwe baharini, inamfaa kuliko kukwaza mmoja tu aliye mwenzao hawa wadogo.#Mat. 18:6-7. 3Jiangalieni! Ndugu yako akikukosea, umtishe! Naye akijuta, umwondolee!#Mat. 18:15. 4Ijapo, akukosee mara saba siku moja na kukurudia mara saba na kusema: Nimejuta, sharti umwondolee!#Mat. 18:21-22.
Mategemeo.
5Mitume wakamwambia Bwana: Tuongezee nguvu za kumtegemea Mungu!#Mar. 9:24. 6Bwana akasema: Cheo chenu cha kumtegemea Mungu kikiwa kidogo kama kipunje cha mbegu, mtauambia mkuyu huu: Ng'oka hapo, ulipo, ujipande baharini! nao utawatii.#Mat. 17:20; 21:21.
Malipo ya mtumwa.
7Kwenu yuko mwenye mtumwa wa kulima au wa kuchunga atakayemwambia huyo, akirudi toka shamba: Sasa hivi njoo, ukae chakulani? 8Hatamwambia: Andalia chakula, nitakachokila, ujifunge nguo, unitumikie, mpaka nitakapokwisha kula na kunywa! Kisha nawe ule, unywe? 9Je? Atamwambia mtumwa asante, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? 10Vivyo nanyi matakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa semeni: Sisi tu watumwa wasiofaa, tumefanya tu yaliyotupasa kuyafanya!
Wenye ukoma kumi.
11*Ikawa, alipokwenda Yerusalemu, akashika njia ya kupita katikati ya Samaria na Galilea.#Luk. 9:51; 13:22. 12Alipoingia kijijini akakutana na waume kumi wenye ukoma waliokuwa wamesimama mbali,#3 Mose 13:45-46. 13wakapaza sauti wakisema: Bwana Yesu, tuhurumie! 14Alipowaona akawaambia: Nendeni kujionyesha kwa watambikaji! Ikawa, walipokwenda wakatakaswa.#Luk. 5:14; 3 Mose 14:2-3. 15Lakini mmoja wao alipoona, ya kuwa amepona, akarudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu. 16Akamwangukia kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. 17Yesu akajibu akisema: Sio kumi waliotakaswa? Wale tisa wako wapi? 18Hawakuonekana wengine waliorudi, wamtukuze Mungu, pasipo huyu mgeni? 19Akamwambia: Inuka, uende zako! Kunitegemea kwako kumekuponya.*#Luk. 7:50.
Siku ya Mwana wa mtu.
20*Alipoulizwa na Mafariseo: Ufalme wa Mungu unakuja lini? akawajibu akisema: Ufalme wa Mungu unapokuja, watu hawatauona kwa macho,#Mat. 12:28; Yoh. 18:36; Rom. 14:17. 21wala hawatasema: Tazama, up hapa! au: Uko huko! Kwani ufalme wa Mungu umo ndani yenu.#Mat. 24:23.
22Kisha akawaambia wanafunzi: Siku zitakuja, mtakapotunukia kuiona siku moja tu ya siku za Mwana wa mtu, msiione. 23Nanyi watu watakapowaambia: Tazameni huko! Tazameni hapa! msiende huko, wala msiwafuate!#Luk. 21:8. 24Kwani kama umeme unavyomulika mbinguni toka pembe hii mpaka pembe ile na kuviangaza vilivyoko chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa mtu, siku yake itakapofika.#Mat. 24:26-27. 25Lakini kwanza imempasa kuteswa mengi na kukataliwa nao wa kizazi hiki.#Luk. 9:22. 26Navyo vilivyokuwa siku za Noa, ndivyo vitakavyokuwa hata siku zile za Mwana wa mtu.#Mat. 24:37-39. 27Walikuwa wakila, hata wakinywa, walikuwa wakioa, hata wakiozwa mpaka siku, Noa alipoingia katika chombo kikubwa, yakaja mafuriko makubwa ya maji, yakawaangamiza wote.#1 Mose 7:7-23. 28Ndivyo, vilivyokuwa hata siku za Loti: walikuwa wakila, hata wakinywa, wakinunua, hata wakiuza, wakipanda, hata wakijenga.#1 Mose 19:15,24-25. 29Lakini siku, Loti alipotoka Sodomu, ndipo, moto uliochanganyika na mawe ya kiberitiberiti ulipotoka mbinguni kama mvua, ukawaangamiza wote. 30Vivyo hivyo vitakuwa siku ile, Mwana wa mtu atakapofunuliwa.* 31Siku ile mtu atakayekuwapo nyumbani juu, vitu vyake vikiwa nyumbani, asiingie kuvichukua! Vivyo hivyo naye atakayekuwako shambani asivirudie vilivyoko nyuma!#Mat. 24:17-18. 32Mkumbukeni mkewe Loti!#1 Mose 19:26. 33Atakayetafuta kuiponya roho yake ataiangamiza; naye atakayeiangamiza ataiponya, iwepo.#Luk. 9:24. 34Nawaambiani: Usiku ule watu wawili watakaolalia kitanda kimoja, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa. 35Wake wawili watakaokuwa wakisaga pamoja, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa.#Mat. 24:40-41. 36Wawili watakaokuwako shambani, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa. 37Walipojibu na kumwuliza: Wapi, Bwana? akawaambia: Penye nyamafu ndipo, nao tai watakapokusanyikia.#Mat. 24:28.

Trenutno izabrano:

Luka 17: SRB37

Istaknuto

Podijeli

Kopiraj

None

Želiš li da tvoje istaknuto bude sačuvano na svim tvojim uređajima? Kreiraj nalog ili se prijavi