YouVersion logo
Dugme za pretraživanje

Mwanzo 6:1-4

Mwanzo 6:1-4 ONMM

Idadi ya watu ilipoanza kuongezeka duniani, na watoto wa kike wakazaliwa kwao, wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua. Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa; siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.” Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na hata baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa wa zamani, na watu mashuhuri.