Mattayo MT. 22
22
1YESU akajibu, akawaambia tena kwa mifano, akinena, 2Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwana wake arusi. 3Akawatuma watumishi wake wawaite walioalikwa kuja arusini: nao hawakutaka kuja. 4Akatuma tena watumishi wengine, akinena, Waambieni wale walioalikwa, Tʼazameni nimeandaa karamu yangu: ngʼombe na vinono vimekwisha kuehinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini. 5Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake: 6nao waliosalia wakawakamata watumishi wake, wakawatenda jeuri, wakawana. 7Bassi yule mfalme alipopata khahari, akaghadhabika: akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. 8Kisha akawaambia watumishi wake. Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. 9Bassi enendeni hatta njia panda za njia kuu, na wote mwaonao waiteni arusini. 10Watumishi wale wakatoka wakaingia njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu na wema: arusi ikajaa wageni. 11Alipoingia yule mfalme kuwatazama wageni, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. 12Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Akatekewa. 13Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono, mchukueni mkamtupe katika giza la nje: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. 14Kwa maana wengi waitwao, wateule wachache.
15Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafauya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno. 16Wakawatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodiano, wakanena, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, ua njia va Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu, kwa maana hutazami sura za watu. 17Bassi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, au si halali? 18Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki? 19Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. 20Akawaambia, Ya nani sanamu hii, na anwani hii? 21Wakamwambia, Ya Kaisari. Akawaambia, Bassi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. 22Waliposikia, wakataajabu, wakamwacha, wakaenda zao. 23Siku ile Masadukayo, watu wanenao kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, 24wakinena, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, nae hana watoto, ndugu yake amwoe mkewe, illi ampatie ndugu yake mzao. 25Bassi, kwetu palikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia ndugu yake nike wake. 26Vivyo hivyo wa pili nae, na wa tatu, hatta wote saba. 27Mwisho wa wote yule mwanamke akafa nae. 28Katika kiyama, hassi, atakuwa mke wa nani katika wale saba? Maana wote walikuwa nae. 29Yesu akajihu, akawaamhia, Mwajidanganya, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. 30Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaozwi, bali huwa kama malaika wa Mungu mbinguni. 31Tena katika khabari ya kiyama ya wafu, hamjaiisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, 32Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, hali wa wahayi. 33Makutano waliposikia, wakashangaa kwa elimu yake.
34Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, wakakusanyika pamoja. 35Mmoja wao, mwana sharia, akamwuliza, akimjaribu; akinena, 36Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38Amri ya kwanza na iliyo kuu ndiyo hii. 39Na ya pili yafanana nayo, ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40Amri hizi mbili yazitegemea torati yote nao manabii.
41Mafarisayo walipokusanyika, Yesu akawauliza, 42akinena, Mwaonaje katika khabari za Kristo? Yu mwana wa nani? Wakamwambia, Wa Daud. 43Akawaambia, Imekuwaje bassi Daud katika Roho kumwita Bwana, akinena,
44Bwana alimwambia Bwana wangu,
Keti mkono wangu wa kuume,
Hatta niwawekapo adui zako chini ya miguu yako?
45Bassi, Daud akimwita Bwana, amekuwaje mwana wake? 46Hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu tangu siku ile kumwuliza neno tena.
Nu markerat:
Mattayo MT. 22: SWZZB1921
Märk
Dela
Kopiera
Vill du ha dina höjdpunkter sparade på alla dina enheter? Registrera dig eller logga in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: