Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mdo 1
BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume
Siku 20
BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.
Tusome Biblia Pamoja (Januari)
Siku 31
Sehemu ya kwanza ya msururu wa sehemu 12, mpango huu huongoza jamii kupitia Biblia yote pamoja kwa siku 365. Waalike wengine kujiunga kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikilizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kila siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na la Kale, pamoja na Zaburi ikiwa imetawanyika kote kote. Sehemu ya kwanza inajumuisha vitabu vya Luka, Matendo, Danieli na Mwanzo.