Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Efe 2:5
Mbona Mungu ananipenda?
Siku 5
Maswali: Ikija kwa Mungu, tuna maswali mengi sana. Kwa sababu ya tamaduni zetu, swali moja ambalo tutajipata tukijiuliza ni, "Mbona Mungu ananipenda?" au "Ni vipi atanipenda?" Mpango huu unashirikisha jumla ya vifungu 26 vya Biblia—Kila kifungu kikiongea juu ya upendo wa Mungu usiokuwa na shaka.
Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako
Siku 6
Kamwe katika historia ya ulimwengu taasisi ya ndoa haijawahi kuwa chini ya chunguzi kama ilivyo. Kila siku, jamii hutafuta kufafanua upya maana ya kuoa, na Wakristo wanakabiliwa na ukosoaji mkubwa zaidi kwa kushikilia kile kinachoitwa mtazamo na wa mawazo finyu kuhusu ndoa. Kwa hivyo kusudi la kibiblia la ndoa ni nini, na tunapaswa kuombaje kama waumini ili kuhifadhi maana yake? Katika kampeni yetu ya siku sita, Maombi ya Kusudi katika Ndoa Yako, wanandoa wanaweza kuomba kuwepo na maana katika ndoa yao wenyewe, na pia kuthibitisha ufahamu wa kimungu wa muungano wa agano kati ya mwanamume na mwanamke.
Upendo wa Kweli ni nini?
Siku 12
Kila mtu anataka kujua upendo ni kitu gani. Lakini watu wachache huangalia ni nini Biblia inasema kuhusu upendo. Upendo ni mada moja muhimu ya Maandiko na pia wema muhimu zaidi katika maisha ya Kikristo. Mpango huu kutoka Huduma za Thistlebend unashughulikia maana ya kibiblia ya upendo na jinsi ya kuboresha kumpenda Mungu na kuwapenda wengine.
Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022
siku 28
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.