Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Isa 43:2

Faraja Ya Majaliwa Ya Mungu
Siku 3
Maisha yana namna ya kukufanya ujisikie kana kwamba umesahaulika. Iwe ni wakati maisha yanapoanza kugeuka kuwa mabaya au wakati mambo yanaonekana hayaendi sawa, Mungu ana mpango na wewe. Katika mpango huu wa siku 3, Tony Evans anafundisha jinsi Mungu anavyodhibiti kila kitu, haijalishi kinaonekana kibaya kiasi gani.

Ibada juu ya Vita vya Akilini
Siku 14
Hii ibada itakusaidia kwa himizo za tumaini la kushinda hasira, machafuko, hukumu, hofu, shaka ... chochote kile. Ufahamu huu utakusaidia kujua njama ya adui ya kukuchanganya na kukudanganya, kukabiliana na mwelekeo wa mawazo ulioharibika, kupata ushindi katika kubadilisha mawazo yako, kupata nguvu, kutiwa moyo na, muhimu zaidi, ushindi juu ya kila vita akilini mwako. Una nguvu ya kupigana ... hata ikiwa ni siku moja kwa wakati!

Imani Juu Ya Hofu
26 Siku
Majira ya Maajilio yanatualika kuandaa mioyo yetu kwa ajili ya kuja kwa Yesu, si kwa sherehe tu bali pia kwa tafakari. Katika simulizi ya Krismasi, hofu ni dhima inayojirudia: hekaluni, kwenye ndoto, milimani na hata kwenye nyumba za utulivu. Lakini kila mara, Mungu hatoi hukumu bali anatupa hakikisho: 'Usiogope.' Katika tafakari fupi fupi za mfululizo huu, tunachunguza jinsi kuchagua imani badala ya hofu kunavyotusaidia kumkaribisha Yesu kwa kina zaidi katika maisha yetu.

Soma Biblia Kila Siku 2 - 2026
28 Siku
Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Februari. Utasoma kitabu cha Isaya na Zaburi. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Isipokuwa imeandikwa vinginevyo, nukuu zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Union Version (SUV).