Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mt 6:33
Fukuza Hofu
Siku 3
Unaweza kushinda hisia za hofu. Dkt. Tony Evans anakuongoza kwenye njia ya uhuru katika mpango huu wa usomaji wa kupata ufahamu. Gundua maisha ya furaha na amani ambayo umekuwa ukitaka, unapotumia kanuni zilizowekwa katika mpango huu.
Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.
Siku 5
Bwana yu hai na ni mkamilifu leo, na uongea na kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu kumuona na kumsikia Mungu. Kupitia kuchunguza hadithi ya safari ya mtu mmoja ya kufahamu sauti ya Mungu katika mabanda ya Nairobi, utasoma vile ilivyo kumsikia na kumfuata Mungu.
Msihangaike
Siku 5
Katika kitabu cha Mathayo 6:24-34 Kristo anaeleza jinsi Injili inadhihirisha sababu hasa tunakumbwa na wasiwasi au mahangaiko, na la muhimu zaidi, Kristo anatuwezesha kuelewa jinsi Injili inavyotuokoa kutokana na uwepo wa wasiwasi au mahangaiko.
Kuomboleza Vyema
Siku 6
Huzuni huja kama sehemu ya asili ya maisha. Unapompoteza mtu unayempenda, inaweza kuwa vigumu kujiongoza katika mchakato wa kuomboleza. Kupitia mpango huu wa kusoma, Tony Evans anazungumza kutoka moyoni mwake kulingana na jinsi alivyompoteza kwa ghafla mpwa wake wa kike. Kanuni hizi zinaweza kukusaidia kujifunza jinsi ya kuomboleza vyema na kukumbatia uponyaji.
Pumua shauku ya kiroho ndani ya ndoa yako
Siku 7
Ikichukuliwa kutoka kitabu chake kipya "Maisha marefu ya upendo", Gary Thomas anaongea kuhusu madhumuni ya milele ndani ya ndoa. Jufunze viungu vya maana kwa kusaidia kubeba ndoa yako ndani ya mahusiano yakujaa na mambo mapya, ikienezwa na maisha kwa wengine.
Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi
Siku 7
Je! unajua Yesu anasema nini kuhusu wasiwasi wetu? Acha. Ndiyo, anatuambia tuiache. Wasiwasi ni moja ya dalili kuu kwamba imani yetu imetikisika na imani yetu iko chini. Wakati wewe au mimi tunakuwa na wasiwasi, tunakosa kuweka imani ifaayo juu ya udhibiti mkuu wa Mungu. Bado sote, bado tunafanya hivyo, sivyo? Ndiyo maana Tony Evans ameweka pamoja mpango wa kusoma wa siku 7 ili kukusaidia WEWE kushinda wasiwasi. Unaweza kuvunja mzunguko na kubadilishana wasiwasi kwa amani.
Mafunzo ya Yesu
Siku 7
Yesu alifunza kuhusu mada nyingi- baraka zinazodumu, uzinzi, maombi na mengi zaidi. Ina maana gani kwa watu wa leo? Video fupi yaeleza kila upande wa hadithi kwa kila siku ya mpango huu.
Mpango Bora wa Kusoma
Siku 28
unajisihisi umezidiwa, kutoridhika, na kukwama maishani? Je unatamani maisha yako ya kila siku yaboreke? Neno la Mungu ni mwongozo kwa siku njema. Katika mpango huu wa siku 28, utagundua njia kutoka kuishi tu maisha mema, hadi kuishi maisha mema ambayo Mungu amekutazamia.
SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20
Siku 31
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.