Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Flp 3:10

Imani
Siku 12
Je, kuona ni kuamini? Au kuamini ni kuona? Hayo ni maswali ya imani. Mpango huu unatoa masomo ya kina kuhusu imani—kutoka kwa hadithi za Agano la Kale kuhusu watu halisia ambao walionyesha imani jasiri katika matukio yasiowezekana kwa mafundisho ya Yesu juu ya somo. Kupitia kwa kusoma kwako, utatiwa moyo ili kudumisha uhusiano wako na Mungu na uwe mfuasi mwenye imani zaidi wa Yesu.

Ahadi za kila siku ya maisha yako
30 Siku
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022
Siku 30
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

Kutana na Yesu
30 Siku
Yesu ni mtu wa aina gani haswa — na je, hata anajali mtu kama mimi? Je, Yesu anaweza kuponya yaliyoporomoka ndani yangu? Kwa nini Yesu anaruhusu mateso? Je, naweza kumfuata Yesu na bado niwe na mashaka? Kumfuata yeye kutanigharimu mimi nini hasa — kuna faida gani? Mpango huu wa masomo ya siku 30, uliopata msukumo kutokana na kipindi cha televisheni cha The Chosen, unaangazia simulizi za walioshuhudia maisha ya Yesu kujibu maswali haya. Iwapo umeanza kuzingatia madai ya Kristo, basi masomo haya ni mahali pazuri pa kuanzia.

Soma Biblia Kila Siku 08/2026
31 Siku
Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Agosti. Utasoma kitabu cha 2 Nyakati na Wafilipi. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Isipokuwa imeandikwa vinginevyo, nukuu zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Union Version (SUV).