1
Isaya 60:1
Neno: Bibilia Takatifu 2025
“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa BWANA umezuka juu yako.
Linganisha
Chunguza Isaya 60:1
2
Isaya 60:3
Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.
Chunguza Isaya 60:3
3
Isaya 60:2
Tazama, giza litaifunika dunia, na giza nene litayafunika mataifa, lakini BWANA atazuka juu yako na utukufu wake utaonekana juu yako.
Chunguza Isaya 60:2
4
Isaya 60:22
Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu, mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu. Mimi ndimi BWANA; katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”
Chunguza Isaya 60:22
5
Isaya 60:19
Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, kwa maana BWANA atakuwa nuru yako ya milele, naye Mungu wako atakuwa utukufu wako.
Chunguza Isaya 60:19
6
Isaya 60:20
Jua lako halitazama tena, nao mwezi wako hautafifia tena; BWANA atakuwa nuru yako milele, nazo siku zako za huzuni zitakoma.
Chunguza Isaya 60:20
7
Isaya 60:5
Ndipo utatazama na kutiwa nuru, moyo wako utasisimka na kujaa furaha, mali iliyo baharini italetwa kwako, utajiri wa mataifa utakujilia.
Chunguza Isaya 60:5
8
Isaya 60:4
“Inua macho yako na utazame pande zote: Wote wanakusanyika na kukujia, wana wako wanakuja toka mbali, nao binti zako wanabebwa mikononi.
Chunguza Isaya 60:4
9
Isaya 60:21
Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu, nao wataimiliki nchi milele. Wao ni chipukizi nililolipanda, kazi ya mikono yangu, ili kuonesha utukufu wangu.
Chunguza Isaya 60:21
10
Isaya 60:18
Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako, wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako, lakini utaita kuta zako Wokovu, na malango yako Sifa.
Chunguza Isaya 60:18
11
Isaya 60:11
Malango yako yatakuwa wazi siku zote, kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku, ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa: wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi.
Chunguza Isaya 60:11
12
Isaya 60:6
Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako, ngamia vijana wa Midiani na Efa. Nao watu wote wanaotoka Sheba watakuja, wakichukua dhahabu na uvumba na kutangaza sifa za BWANA.
Chunguza Isaya 60:6
13
Isaya 60:10
“Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonesha huruma.
Chunguza Isaya 60:10
14
Isaya 60:15
“Ingawa umeachwa na kuchukiwa, bila yeyote anayesafiri ndani yako, nitakufanya kuwa fahari ya milele, na furaha ya vizazi vyote.
Chunguza Isaya 60:15
15
Isaya 60:16
Utanyonya maziwa ya mataifa, na kunyonyeshwa matiti ya wafalme. Ndipo utakapojua kwamba Mimi, BWANA, ni Mwokozi wako, Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.
Chunguza Isaya 60:16
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video