Lakini Mungu huwadumisha wenye uwezo kwa nguvu zake;
Huinuka, wasiokuwa na tumaini la kuishi.
Huwapa kuwa na salama, nao wapumzika kwayo;
Na macho yake ya juu ya njia zao.
Wao wametukuzwa; lakini kitambo kidogo hutoweka;
Naam, hushushwa, na kuondolewa njiani kama wengine wote,
Nao hukatwa kama vile masuke ya ngano.