1
Yakobo 3:17
Swahili Revised Union Version
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Linganisha
Chunguza Yakobo 3:17
2
Yakobo 3:13
Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aoneshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
Chunguza Yakobo 3:13
3
Yakobo 3:18
Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Chunguza Yakobo 3:18
4
Yakobo 3:16
Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
Chunguza Yakobo 3:16
5
Yakobo 3:9-10
Kwa huo tunamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo unwawalaani wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
Chunguza Yakobo 3:9-10
6
Yakobo 3:6
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.
Chunguza Yakobo 3:6
7
Yakobo 3:8
Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
Chunguza Yakobo 3:8
8
Yakobo 3:1
Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.
Chunguza Yakobo 3:1
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video