1
Luka 6:38
Swahili Revised Union Version
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Linganisha
Chunguza Luka 6:38
2
Luka 6:45
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Chunguza Luka 6:45
3
Luka 6:35
Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
Chunguza Luka 6:35
4
Luka 6:36
Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
Chunguza Luka 6:36
5
Luka 6:37
Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; sameheni, nanyi mtasamehewa.
Chunguza Luka 6:37
6
Luka 6:27-28
Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
Chunguza Luka 6:27-28
7
Luka 6:31
Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.
Chunguza Luka 6:31
8
Luka 6:29-30
Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.
Chunguza Luka 6:29-30
9
Luka 6:43
Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri
Chunguza Luka 6:43
10
Luka 6:44
kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.
Chunguza Luka 6:44
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video