1
Luka 6:38
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Wapeni wengine vitu, nanyi mtapokea. Mtapewa vingi; kipimo chenye ujazo wa kusukwasukwa na kumwagika. Mungu atawapa ninyi kwa kadri mnavyotoa.”
Linganisha
Chunguza Luka 6:38
2
Luka 6:45
Watu wema wana mambo mazuri katika mioyo yao. Ndiyo sababu hutamka mambo mema. Lakini waovu wana mioyo iliyojaa uovu, na ndiyo sababu hutamka mambo maovu. Mambo wanayotamka watu katika midomo yao, ndiyo yaliyojaa katika mioyo yao.
Chunguza Luka 6:45
3
Luka 6:35
Ninawaambia kuwa wapendeni adui zenu na kuwatendea mema. Wakopesheni watu bila kutarajia kitu kutoka kwao. Mkifanya hivyo, mtapata thawabu kuu. Mtakuwa wana wa Mungu Mkuu Aliye Juu. Ndiyo kwa sababu Mungu ni mwema hata kwa wenye dhambi na wasiomshukuru.
Chunguza Luka 6:35
4
Luka 6:36
Iweni na upendo na huruma, kama Baba yenu alivyo.
Chunguza Luka 6:36
5
Luka 6:37
Msiwahukumu wengine, nanyi hamtahukumiwa na Mungu. Msiwalaani wengine nanyi hamtalaaniwa. Wasameheni wengine nanyi mtasamehewa.
Chunguza Luka 6:37
6
Luka 6:27-28
Lakini ninawaambia ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wale wanaowachukia. Mwombeni Mungu awabariki wale wanaowalaani ninyi, waombeeni wale wanaowaonea.
Chunguza Luka 6:27-28
7
Luka 6:31
Watendeeni wengine kama mnavyotaka wao wawatendee ninyi.
Chunguza Luka 6:31
8
Luka 6:29-30
Mtu akikupiga shavu moja, mwache akupige na la pili pia. Mtu akichukua koti lako, usimkataze kuchukua shati pia. Mpe kila akuombaye kitu. Mtu yeyote akichukua kitu chako, usitake akurudishie.
Chunguza Luka 6:29-30
9
Luka 6:43
Mti mzuri hauzai matunda mabaya. Na mti mbaya hauzai matunda mazuri.
Chunguza Luka 6:43
10
Luka 6:44
Kila mti unatambuliwa kutokana na aina ya matunda unayozaa. Huwezi kupata tini kwenye vichaka vya miiba. Na huwezi kuchuma zabibu kwenye michongoma!
Chunguza Luka 6:44
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video