1
Marko 6:31
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Kisha Yesu akawaambia, “Njooni mnifuate peke yenu hadi mahali patulivu na palipo mbali na watu wengine ili mpumzike kidogo”, kwani pale walikuwepo watu wengi wakija na kutoka, nao hawakuwa na nafasi ya kula.
Linganisha
Chunguza Marko 6:31
2
Marko 6:4
Yesu akawaambia, “kila mtu humheshimu nabii isipokuwa watu wa mji wa kwao mwenyewe, jamaa zake mwenyewe na wale wa nyumbani mwake mwenyewe.”
Chunguza Marko 6:4
3
Marko 6:34
Alipotoka katika mashua, Yesu aliona kundi kubwa, na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji, Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.
Chunguza Marko 6:34
4
Marko 6:5-6
Yesu hakuweza kufanya miujiza ya aina yoyote pale, isipokuwa aliweka mikono juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. Naye akashangazwa na jinsi watu wa mji wa kwao mwenyewe walivyokosa kuwa na imani. Kisha Yesu alizunguka vijijini akiwafundisha watu.
Chunguza Marko 6:5-6
5
Marko 6:41-43
Akachukua ile mikate mitano na samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akashukuru na akaimega. Akawapa wanafunzi wake ili wawape watu. Pia aligawanya samaki wawili miongoni mwao wote. Wakala na wote wakatosheka. Wakachukua mabaki ya vipande vya mikate na samaki na kujaza vikapu kumi na viwili.
Chunguza Marko 6:41-43
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video