Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa hekalu, akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kwa maana imeandikwa:
‘Atawaamuru malaika wake wakulinde,’
na tena,
‘Watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa mguu kwenye jiwe.’”
Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”