1
Yohana 15:5
Swahili Roehl Bible 1937
Mimi ni mzabibu, ninyi m matawi. Anayekaa ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa mengi. Kwani pasipo mimi hamna mwezacho kukifanya.
Linganisha
Chunguza Yohana 15:5
2
Yohana 15:4
Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu! Kama tawi lisivyoweza kuzaa likiwa peke yake, lisipokaa mzabibuni, vivyo hivyo nanyi hamna mwezacho, msipokaa ndani yangu.
Chunguza Yohana 15:4
3
Yohana 15:7
Mtakapokaa ndani yangu, nayo maneno yangu yatakapokaa ndani yenu, mtaomba lo lote, mnalolitaka, kisha mtalipata.
Chunguza Yohana 15:7
4
Yohana 15:16
Sio ninyi mlionichagua, lakini ndiye mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka, mwende kuzaa matunda, nayo matunda yenu yakae; kwa hiyo Baba atawapa lo lote, mtakalomwomba katika Jina langu.*
Chunguza Yohana 15:16
5
Yohana 15:13
Hakuna mwenye upendo kumpita mwenye kujitoa, awaokoe wapenzi wake.
Chunguza Yohana 15:13
6
Yohana 15:2
Kila tawi langu lisilozaa huliondoa; lakini kila tawi lizaalo hulitakasa akilipogoa, lipate kuzaa mengi.
Chunguza Yohana 15:2
7
Yohana 15:12
Hili ndilo agizo langu: Mpendane, kama nilivyowapenda!
Chunguza Yohana 15:12
8
Yohana 15:8
Hapo ndipo, Baba yangu anapotukuzwa, mnapozaa mengi, mkawa wanafunzi wangu.*
Chunguza Yohana 15:8
9
Yohana 15:1
*Mimi ni mzabibu wa kweli naye Baba yangu ndiye mpalilizi.
Chunguza Yohana 15:1
10
Yohana 15:6
Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi, likikauka; kisha watu huyakusanya pamoja na kuyatupa motoni yateketee.
Chunguza Yohana 15:6
11
Yohana 15:11
Nimewaambia haya, furaha yangu iwakalie, nanyi furaha yenu itimie yote.
Chunguza Yohana 15:11
12
Yohana 15:10
Mtakapoyashika maneno yangu mtakaa na kunipenda, kama mimi nilivyoyashika maagizo ya Baba yangu, nikakaa na kumpenda yeye.
Chunguza Yohana 15:10
13
Yohana 15:17
Haya nawaagizani: Mpendane!
Chunguza Yohana 15:17
14
Yohana 15:19
Kama mngekuwa wa ulimwengu, wao wa ulimwengu wangewapenda, kwamba m wenzao. Lakini kwa sababu ham wa ulimwengu, kwani mimi naliwachagua na kuwatoa ulimwenguni, kwa hiyo wao wa ulimwengu huwachukia.
Chunguza Yohana 15:19
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video