1
Yohana 6:35
Swahili Roehl Bible 1937
Yesu akawaambia: Mimi ndio mkate wa uzima; ajaye kwangu hataona njaa, naye anitegemeaye hataona kiu hata siku moja.
Linganisha
Chunguza Yohana 6:35
2
Yohana 6:63
Roho ndiyo inayotupatia uzima, mwili haufai kitu. Maneno, niliyowaambia, ndiyo ya Kiroho yenye uzima.
Chunguza Yohana 6:63
3
Yohana 6:27
Sumbukieni vyakula! Lakini vile vinavyoangamia sivyo, ni vile vinavyokaa, viwafikishe penye uzima wa kale na kale, navyo ndivyo, Mwana wa mtu atakavyowapani ninyi. Kwani huyu ndiye, Baba Mungu aliyemwagiza hivyo na kumtia muhuri.
Chunguza Yohana 6:27
4
Yohana 6:40
Kwani haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu: kila anayemtazamia Mwana na kumtegemea apate uzima wa kale na kale, nami nitamfufua siku ya mwisho.
Chunguza Yohana 6:40
5
Yohana 6:29
Yesu akajibu, akawaambia: Hii ndiyo kazi ya Mungu, mkimtegemea yeye, aliyemtuma.*
Chunguza Yohana 6:29
6
Yohana 6:37
Wote, Baba anipao, ndio watakaokuja kwangu; naye ajaye kwangu sitamfukuza, ajiendee.
Chunguza Yohana 6:37
7
Yohana 6:68
ndipo, Simoni Petero alipomjibu: Bwana, tumwendee nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa kale na kale.
Chunguza Yohana 6:68
8
Yohana 6:51
Mimi ndio mkate wenye uzima ulioshuka toka mbinguni. Mtu atakayeula mkate huu atakuwa mzima pasipo mwisho. Nao mkate, nitakaowapa mimi, ndio mwili wangu utakaotolewa, ulimwengu upate uzima.
Chunguza Yohana 6:51
9
Yohana 6:44
Hakuna awezaye kuja kwangu, Baba aliyenituma asipomvuta, nami nitamfufua siku ya mwisho.
Chunguza Yohana 6:44
10
Yohana 6:33
Kwani mkate wa Mungu ndio ule ushukao toka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.
Chunguza Yohana 6:33
11
Yohana 6:48
Mimi ndio mkate wa uzima.
Chunguza Yohana 6:48
12
Yohana 6:11-12
Kisha Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia waliokaa; vile vile navyo visamaki, kama walivyotaka. Lakini waliposhiba, akawaambia wanafunzi wake: Yakusanyeni makombo yaliyosalia, pasipatikane kinachopotea!
Chunguza Yohana 6:11-12
13
Yohana 6:19-20
Walipokwisha endelea mwendo wa nusu saa na kupita kidogo, wakamwona Yesu, anavyokwenda juu ya bahari na kukifikia chombo karibu, wakaogopa. Ndipo, alipowaambia: Ni miye, msiogope!
Chunguza Yohana 6:19-20
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video