Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Mwenye hekima asijivunie nguvu zake,
wala tajiri asijivunie utajiri wake.
Anayetaka kujivuna na ajivunie jambo hili:
Kwamba ananifahamu
kwamba anajua Mwenyezi-Mungu hutenda mema,
hufanya mambo ya haki na uadilifu duniani.
Watu wa namna hiyo ndio wanipendezao.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”