Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Timotheo Utangulizi

Utangulizi
Nyaraka za 1 na 2 Timotheo na ule wa Tito zinatambuliwa kama nyaraka za kichungaji zilizoandikwa na Paulo. Alimwandikia Timotheo msaidizi wake, ambaye alikuwa amemwacha huko Efeso kusahihisha matatizo kadhaa kuhusu mwenendo wa kanisa, uongozi wa kanisa, na mambo yaliyowahusu waumini. Paulo aliandika ili kumpa Timotheo maagizo kuhusu mambo haya, ili kanisa lifanye kazi yake vyema. Aliandika pia kumtia moyo Timotheo asichoke katika maisha yake ya Kikristo, bali aishi maisha ya ukamilifu kwa utukufu wa Mungu.
Timotheo alizaliwa huko Listra. Baba yake alikuwa Myunani, naye mama yake Myahudi ambaye alimfundisha Maandiko tangu utoto. Paulo alipofika Listra katika safari yake ya pili ya kitume, alimchagua Timotheo ambaye alishirikiana naye hadi mwisho wa huduma yake.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kumtia moyo na kumpa maelekezo Timotheo, ambaye alikuwa kiongozi mchanga, kuhusu utaratibu wa kanisa, imani na maadibisho.
Mahali
Pengine Filipi.
Tarehe
Kama mwaka wa 64 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo na Timotheo.
Wazo Kuu
Umuhimu wa kuwa na imani sahihi, mwenendo mnyofu, na pia uadilifu.
Mambo Muhimu
Kumwelekeza Timotheo kuhusu sifa na wajibu wa viongozi mbalimbali katika kanisa, na kumpa mwongozo katika wajibu wake wa kichungaji.
Mgawanyo
Maonyo kuhusu mafundisho ya uongo (1:1-20)
Mafundisho kuhusu maombi (2:1-15)
Sifa zinazowapasa waangalizi na wazee wa kanisa (3:1-16)
Maonyo na huduma (4:1–5:25)
Huduma ya Kikristo, na maagizo kwa Timotheo (6:1-21).

Iliyochaguliwa sasa

1 Timotheo Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia