Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wakorintho 3:12-18

2 Wakorintho 3:12-18 NENO

Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana. Sisi si kama Musa, ambaye ilimpasa kuweka utaji wa kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mng’ao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka. Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana hadi leo utaji ule ule hufunika Torati inaposomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Al-Masihi peke yake unaondolewa. Hata leo Torati ya Musa inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao. Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana Mungu Mwenyezi, utaji unaondolewa. Basi Bwana Isa ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi, hapo pana uhuru. Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji, tunadhihirisha utukufu wa Bwana Isa kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, unaotoka kwa Bwana Isa, aliye Roho.