2 Wathesalonike 1:1-4
2 Wathesalonike 1:1-4 NENO
Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kundi la waumini la Wathesalonike mlio katika Mungu, Baba yetu, na Bwana Isa Al-Masihi. Neema na amani zinazotoka kwa Mungu Baba Mwenyezi na kwa Bwana Isa Al-Masihi ziwe nanyi. Ndugu, inatupasa kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, na inastahili hivyo kwa sababu imani yenu inazidi kukua sana, nao upendo wa kila mmoja wenu kwa mwenzake unazidi kuongezeka. Ndiyo sababu miongoni mwa makundi ya waumini ya Mungu, tunajivunia saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.