Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 6:8-10

Matendo 6:8-10 NENO

Stefano, akiwa amejaa neema na nguvu za Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa miongoni mwa watu. Hata hivyo, ukainuka upinzani wa watu wa Sinagogi la Watu Huru (kama lilivyokuwa linaitwa) la Wayahudi wa Kirene na wa Iskanderia, na wengine kutoka Kilikia na jimbo la Asia. Watu hawa wakaanza kupingana na Stefano. Lakini hawakuweza kushindana na ile hekima aliyopewa na Roho wa Mungu alipokuwa akisema.