Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 26:5-11

Kumbukumbu 26:5-11 NEN

Kisha utatangaza mbele za BWANA Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi. Lakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu. Kisha tulimlilia BWANA, Mungu wa baba zetu, naye BWANA akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu. Kwa hiyo BWANA akatutoa nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, pamoja na utisho mkuu, ishara za miujiza na maajabu. Akatuleta mahali hapa akatupa nchi hii, nchi inayotiririka maziwa na asali; nami sasa ninaleta malimbuko ya ardhi ambayo wewe, Ee BWANA, umenipa.” Weka kapu mbele za BWANA Mungu wako na usujudu mbele zake. Kisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walioko miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyo BWANA Mungu wenu amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu.