Wagalatia 1:6-9
Wagalatia 1:6-9 NENO
Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Al-Masihi na kuifuata Injili nyingine, ambayo kwa kweli si Injili kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya na wanaotaka kuipotosha Injili ya Al-Masihi. Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri Injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele! Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu yeyote atawahubiria Injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!