Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 13:14-18

Mwanzo 13:14-18 NEN

Baada ya Loti kuondoka BWANA akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.” Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengea BWANA madhabahu.