Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania 7:18-25

Waebrania 7:18-25 NEN

Kwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa (kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu. Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia: “BWANA ameapa naye hatabadilisha mawazo yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’ ” Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Basi pamekuwepo na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani. Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu. Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Waebrania 7:18-25