Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania Utangulizi

Utangulizi
Waraka kwa Waebrania unajulikana kama kitabu cha mambo yaliyo bora, kwa sababu unazungumzia ukuu wa Kristo na kumdhihirisha kama ufunuo wa mwisho wa Mungu. Unabii na ahadi zilizoandikwa katika Agano la Kale zimetimizwa katika Agano Jipya, Kristo akiwa Mpatanishi. Kristo pia athibitishwa kuwa mkuu zaidi ya manabii, malaika, na Mose (ambaye alikuwa mpatanishi wa agano la hapo awali).
Msomaji ameonywa asidharau wala kukataa wokovu mkuu uliotolewa kupitia kwake Kristo. Uwezekano mkubwa ni kwamba waraka huu ulielekezwa kwa Wakristo Wayahudi huko Palestina au Rumi, waliokuwa wanajaribiwa kugeukia tena dini ya Kiyahudi, au kuifanya Injili iwe yenye mfumo wa dini ya Kiyahudi.
Mwandishi
Ingawa waraka hauna jina la mwandishi, una ushahidi mwingi kwamba alikuwa mtu wa kizazi cha pili cha Wakristo aliyekuwa na ujuzi sana wa Agano la Kale.
Kusudi
Mwandishi anamwonyesha Yesu kuwa ndiye ukamilifu wa ufunuo ulionenwa kwanza na Mungu, na kisha na manabii wake.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Kabla ya kuharibiwa kwa Hekalu la Yerusalemu mwaka wa 70 B.K.
Wahusika Wakuu
Yesu, Yoshua, Mose, Melkizedeki, Abrahamu, makuhani, malaika, na watu wenye imani wa Agano la Kale.
Wazo Kuu
Kiini cha Waebrania ni mamlaka na uweza wa Yesu Kristo kama Mjumbe wa neema ya Mungu. Kitabu hiki kinatoa sifa za majina ya heshima zaidi ya ishirini yaliyomtaja Yesu Kristo katika huduma ya ukuhani na ya ufalme.
Mambo Muhimu
Yesu Kristo ni mngʼao wa utukufu wa Mungu, na pia Kristo ni mkuu kuliko malaika, mkuu kuliko viongozi wote, na mkuu kuliko makuhani.
Mgawanyo
Mnenaji bora kwa ajili ya Mungu (1:1–4:13)
Mwombezi au Kuhani aliye bora (4:14–7:28)
Agano na Dhabihu iliyo bora (8:1–10:18)
Agizo la kuitunza na kuilinda imani (11:1–12:29)
Mwisho: Kanuni za maisha ya Kikristo, na maelezo ya binafsi (13:1-25).

Iliyochaguliwa sasa

Waebrania Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia