Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 1:1-5

Hosea 1:1-5 NENO

Neno la Mwenyezi Mungu lililomjia Hosea mwana wa Beeri wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na wakati wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi, mfalme wa Israeli. Mwenyezi Mungu alipoanza kuzungumza kupitia Hosea, Mwenyezi Mungu alimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia ya uzinzi wa kupindukia kwa kumwacha Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo alimwoa Gomeri binti Diblaimu, naye akachukua mimba na kumzalia Hosea mwana. Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Hosea, “Mwite jina Yezreeli, kwa kuwa kitambo kidogo nitaiadhibu nyumba ya Yehu kwa ajili ya mauaji ya kule Yezreeli, nami nitaukomesha ufalme wa Israeli. Katika siku ile nitavunja upinde wa Israeli katika Bonde la Yezreeli.”