Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kimepewa jina la Yeremia, mwana wa kuhani, aliyezaliwa katika kijiji cha Anathothi. Kitabu hiki kinatoa taarifa kwa kina na mtazamo wa kidini, na hali ya kisiasa katika Yuda kwenye kipindi cha miaka arobaini kabla ya kuharibiwa kwa Yerusalemu. Mengi yanajulikana kuhusu historia binafsi ya Yeremia kuliko nabii mwingine yeyote katika Agano la Kale. Yeremia, kama Isaya, alikuwa kijana ambaye aliitwa na Mungu kuionya Yuda juu ya uovu wake.
Kwa miaka 21 ya mwanzo ya huduma ya Yeremia, Yuda, chini ya utawala wa Yosia, walipata mwamko wa kisiasa na uamsho wa kiroho; wakati huo dola ya Waashuru ilikuwa inadidimia. Yeremia alipoanza huduma yake ya unabii 627 K.K., alipata miaka mizuri ya huduma yake hadi Yosia alipouawa mnamo 609 K.K.
Baada ya Yosia kufa, Yeremia alikuwa katika hatari kubwa kutoka kwa viongozi wa dini na wa kisiasa ambao walikasirishwa na ujumbe wake. Ingawa Yeremia alishauri Wayahudi wajitolee kwa Wababeli, wao waliasi. Hivyo mnamo mwaka wa 586 K.K., mji wa Yerusalemu pamoja na Hekalu lake vikaharibiwa, naye Yeremia akachukuliwa kwa nguvu na watu wa Yuda, wakaenda naye Misri.
Mwandishi
Nabii Yeremia.
Kusudi
Yeremia anawaita watu wa Mungu kugeuka kutoka dhambi zao na kumrudia Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
627–586 K.K.
Wahusika Wakuu
Wafalme wa Yuda: Yosia, Yehoahazi, Yehoyakimu, Yehoyakini na Sedekia; Yeremia, Baruku, Ebed-Meleki, Mfalme Nebukadneza, Warekabi.
Wazo Kuu
Uovu usipotubiwa husababisha taifa, jamii, au mtu binafsi kuangamia.
Mambo Muhimu
Yeremia aliorodhesha dhambi za Yuda zote na kutoa unabii wa hukumu ya Mungu, na pia kuwaita watu watubu. Lakini watu waliendelea na maisha yao ya ubinafsi na kuabudu sanamu. Pia viongozi wote walikataa sheria ya Mungu, wakakubaliana na manabii wa uongo. Yerusalemu iliharibiwa, Hekalu likaachwa likiwa magofu, nao watu wakatekwa na kupelekwa uhamishoni Babeli. Ilipasa watu waajibike kwa ajili ya uharibifu na utekwaji huu uliosababishwa na wao kutosikia na kutotii ujumbe wa Mungu.
Mgawanyo
Wito wa Yeremia (1:1-9)
Hali ya dhambi ya Yuda (2:1–6:30)
Hekalu, sheria na agano (7:1–12:17)
Uhakika wa kutekwa (13:1–18:23)
Yeremia anakumbana na viongozi (19:1–29:32)
Ahadi ya kufanywa upya (30:1–33:26)
Ufalme unasambaratika (34:1–39:18)
Safari ya kwenda Misri (40:1–45:5)
Jumbe kuhusu mataifa ya kigeni (46:1–51:64)
Kuanguka kwa Yerusalemu (52:1-34).

Iliyochaguliwa sasa

Yeremia Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia