Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 13:31-38

Yohana 13:31-38 NENO

Baada ya Yuda kutoka nje, Isa akasema, “Sasa Mwana wa Adamu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. Ikiwa Mungu ametukuzwa ndani ya Mwana, Mungu atamtukuza Mwana ndani yake mwenyewe, naye atamtukuza mara moja. “Watoto wangu, mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, vivyo hivyo sasa nawaambia na ninyi: Niendako, ninyi hamwezi kuja. “Amri mpya nawapa: Mpendane. Kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. Mkipendana ninyi kwa ninyi kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.” Simoni Petro akamuuliza, “Bwana, unaenda wapi?” Isa akamjibu, “Ninakoenda huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.” Petro akamuuliza tena, “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Mimi niko tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako.” Isa akamjibu, “Je, ni kweli uko tayari kuutoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin nakuambia, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”