Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoeli Utangulizi

Utangulizi
Yoeli mwana wa Pethueli maana ya jina lake ni “Mwenyezi Mungu ni Mwenyezi Mungu”. Nyingi ya kumbukumbu zake katika kitabu hiki na huduma yake hekaluni zinaonesha kwamba alikuwa nabii aliyetumwa kwa Yuda na Yerusalemu. Kutokana na huduma yake, wengi wamemdhania kuwa nabii wa “kikuhani” (linganisha Yeremia 28:1, 5) aliyenena neno la kweli la Bwana.
Tukio hili lilitafsiriwa kuwa ni pigo kwa sababu ya dhambi za watu. Yoeli alilitafsiri tukio hili kuwa ni kielelezo cha ujio wa “siku ya Mwenyezi Mungu”, yaani siku ya hukumu. Tukio hili la nzige lilileta maombolezo makubwa katika nchi ya Palestina na kupelekea makuhani kulia kilio kikuu. Hata hivyo, kitabu kinaonesha kuwa tukio la nzige halikuwa neno la mwisho kwani baada ya maombolezo makubwa, watu walifarijiwa kwa kuahidiwa kupata furaha kuu. Akiwaonya watu wamgeukie Mwenyezi Mungu kwa toba, Yoeli anatangaza kwamba “siku ya Mwenyezi Mungu” inakuja kwa ajili ya hukumu. Lakini Yoeli anaonesha kuwa kabla siku ya hukumu haijatimia, Mwenyezi Mungu atatuma Roho wake Mtakatifu ili kuleta baraka. Katika tukio la nzige, Yoeli aliona ishara ya hukumu ya mwisho, hivyo akawaonya watu watubu na kumrudia Mwenyezi Mungu.
Mwandishi
Yoeli mwana wa Pethueli.
Kusudi
Kuonya Yuda juu ya hukumu ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa karibu kwa sababu ya dhambi zake; na kuwahimiza watu wamrudie Mwenyezi Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 835–796 K.K.
Wahusika Wakuu
Yoeli na watu wa Yuda.
Wazo Kuu
Hukumu na kumrudia Mwenyezi Mungu.
Mambo Muhimu
Pigo la nzige, kuwaonya watu watubu, na tumaini kwa watu wa Mwenyezi Mungu.
Yaliyomo
Kuvamiwa na nzige (1:1–2:17)
Maonyo na baraka za Mwenyezi Mungu (2:18–3:12).

Iliyochaguliwa sasa

Yoeli Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia