Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo 3:34-44

Maombolezo 3:34-44 NEN

Kuwaponda chini ya nyayo wafungwa wote katika nchi, Kumnyima mtu haki zake mbele za Aliye Juu Sana, kumnyima mtu haki: Je, Bwana asione mambo kama haya? Nani awezaye kusema nalo likatendeka kama Bwana hajaamuru? Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana ndiko yatokako maafa na mambo mema? Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake? Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie BWANA Mungu. Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu kwa Mungu mbinguni, na tuseme: “Tumetenda dhambi na kuasi nawe hujasamehe. “Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia; umetuchinja bila huruma. Unajifunika mwenyewe kwa wingu, ili pasiwe na ombi litakaloweza kupenya.