Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo Utangulizi

Utangulizi
Jina la kitabu hiki ni “Ekah” kwa Kiebrania, maana yake “Jinsi gani.” Maombolezo ni wimbo wa maziko wa kuomboleza Yerusalemu na kuharibiwa kwa Hekalu. Nchi iliachwa bila mfalme, na watu walikuwa wamepelekwa utumwani. Mungu alikuwa amewaonya kuwa wangeenda utumwani wakimwacha.
Yeremia aliandika maombolezo haya kuonyesha huzuni yake kubwa na kuchomwa moyo kwa sababu ya uharibifu wa kutisha wa Yerusalemu. Maafa haya yalihusisha anguko la kuaibisha la utawala wa ukoo wa Daudi, kuangamizwa kabisa kwa kuta za mji na Hekalu, jumba la mfalme na mji kwa ujumla, na mwishowe kupelekwa mbali sana kwa mateka wengi huko Babeli.
Mwandishi
Mapokeo na maandishi ya Kiyahudi na ya Kikristo husema ni Yeremia.
Kusudi
Kuwafundisha watu kwamba kutomtii Mungu huleta maangamizi.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
586–585 K.K.
Wahusika Wakuu
Yeremia, na watu wa Yerusalemu.
Wazo Kuu
Kutafakari mateso na matumaini kwa Mungu.
Mambo Muhimu
Yeremia auomboleza mji wa Yerusalemu, Mungu kugadhibishwa na dhambi, na hali ya kuwa na tumaini katika mateso.
Mgawanyo
Kuangamizwa kabisa kwa Yerusalemu (1:1-22)
Hasira ya Mungu, na kutafuta faraja (2:1-22)
Kutafakari mateso, na kuweka matumaini kwa Mungu (3:1-66)
Utukufu wa awali wa Yerusalemu, na hali ya sasa ya ukiwa (4:1-22)
Kumwomba Mungu aonyeshe huruma (5:1-22).

Iliyochaguliwa sasa

Maombolezo Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia