Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo Utangulizi

Utangulizi
Jina la kitabu hiki ni “Ekah” kwa Kiebrania, maana yake “Jinsi gani”. Maombolezo ni wimbo wa maziko wa kuomboleza Yerusalemu na kuharibiwa kwa Hekalu. Nchi iliachwa bila mfalme, na watu walikuwa wamepelekwa utumwani. Mwenyezi Mungu alikuwa amewaonya kuwa wangeenda utumwani wakimwacha.
Yeremia aliandika maombolezo haya kuonesha huzuni yake kubwa na kuumia moyoni kwa sababu ya uharibifu wa kutisha wa Yerusalemu. Maafa haya yalihusisha anguko la kuaibisha la utawala wa ukoo wa Daudi, kuangamizwa kabisa kwa kuta za mji, Hekalu, jumba la mfalme, na mji wote. Mwishowe walipelekwa uhamishoni Babeli.
Mwandishi
Mapokeo na maandishi ya Kiyahudi na ya Kikristo husema ni Yeremia.
Kusudi
Kuwafundisha watu kwamba kutomtii Mwenyezi Mungu huleta maangamizi.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 586–585 K.K.
Wahusika Wakuu
Yeremia, na watu wa Yerusalemu.
Wazo Kuu
Kutafakari mateso na matumaini kwa Mwenyezi Mungu.
Mambo Muhimu
Yeremia auomboleza mji wa Yerusalemu, Mwenyezi Mungu kugadhibishwa na dhambi, na hali ya kuwa na tumaini katika mateso.
Yaliyomo
Kuangamizwa kabisa kwa Yerusalemu (1:1-22)
Hasira ya Mwenyezi Mungu, na kutafuta faraja (2:1-22)
Kutafakari mateso, na kuweka matumaini kwa Mwenyezi Mungu (3:1-66)
Utukufu wa awali wa Yerusalemu, na hali ya sasa ya ukiwa (4:1-22)
Kumwomba Mwenyezi Mungu aoneshe huruma (5:1-22).

Iliyochaguliwa sasa

Maombolezo Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia